YANGA WANAVYOKWENDA KUKUTANA NA WAAMUZI KUTOKA GUINEA
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetaja mwamuzi wa mechi ya MC Alger dhidi ya Yanga kuwa ni Yakhouba Keita raia wa Guinea.
Yanga wanatarajiwa kuvaana na MC Alger katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, kesho nchini Algeria.
Waamuzi wa pembeni ni Aboubacar Doumbouya na Mamady Tere wote kutoka Guinea.
Yanga,
jana ilitarajiwa kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo huo wakiwa na
msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi, kwa ndege ya
shirika la Emirates kupitia Dubai.