YANGA WAKESHA CCM KIRUMBA WAKIWALINDA MBAO WASIFANYE YAO USIKU
Kama wewe unaichukulia poa mechi ya Mbao FC dhidi ya Yanga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho, basi unajidanganya.
Mechi
hiyo inapigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na
mashabiki wa Yanga maarufu kama “Makomandoo” wameamua kuulinda uwanja
huo.
Mashabiki
hao wameondoka usiku wa kuamkia leo wakiulinda uwanja huo, usiku kucha
ili kuhakikisha Mbao FC na wanaweza kuwasaidia kufanya figisu,
hawafanikiwi hata kidogo.
Hii inaonyesha namns gani Yanga ambao ni mabingwa watetezi walivyopania kuishinda Mbao FC na kutinga fainali.