KIZUNGUMKUTI KINGINE CHA NGOMA NA YANGA HIKI HAPA, YAELEZWA KATIMKIA SAUZI
Mshambuliaji
wa Yanga, Donald Ngoma, ameendelea kuivuruga timu hiyo na safari hii
imeelezwa ameondoka nchini na kuelekea Afrika Kusini bila ya kutoa
taarifa kwa uongozi.
Ngoma,
hivi karibuni aliingia kwenye mtafaruku na viongozi, pia mashabiki wa
timu hiyo akidai ana majeraha huku taarifa zikiwepo yupo fiti na amegoma
kwa makusudi kucheza.
Mshambuliaji
huyo, tayari amekosa michezo kadhaa ya Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na
ile ya kimataifa kutokana na majeraha ya goti, nyonga.
Kwa
mujibu wa vyanzo mshambuliaji huyo ameondoka nchini mwenyewe na
kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kujitibu majeraha hayo, lakini
viongozi wanaonekana kutojua kwa ufasaha kuhusiana na hilo.
Mtoa
taarifa huyo alisema Ngoma akiwa nchini humo atatumia gharama zake kwa
ajili ya kujitibia licha ya kuwepo makundi mbalimbali ya mitandao ya
WhatsApp waliokuwa wakichangishana kwa ajili ya kumtibia yeye na beki
raia wa Togo, Vincent Bossou.
“Tumepata
taarifa za Ngoma kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kwenda
kujitibia majeraha ya goti na nyonga iliyokuwa inamsababishia azikose
baadhi ya mechi za michuano ya kimataifa, ligi kuu na Kombe la FA.
“Tumesikia
anakwenda kujigharamia mwenyewe matibabu yake wakati uongozi na baadhi
ya mashabiki walikuwa wanachangishana kwa ajili ya kufanikisha matibabu
yake huko Sauzi, hivyo tumeshangazwa na mshambuliaji huyo,” kilisema
chanzo cha taarifa.
Alipotafutwa
Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, kuzungumzia hilo, alisema:
“Hizo taarifa ninazisikia kama wewe ulivyosikia, sina taarifa rasmi juu
ya safari yako hiyo.”
Naye
Daktari Mkuu wa Yanga, Edward Bavu alisema: "Sijapata taarifa rasmi za
Ngoma kuondoka, nilizisikia taarifa hizo za kuondoka lakini hajaniambia
na kama ameondoka basi alitakiwa aniambie, ngoja nifuatilie halafu
nitakupa taarifa rasmi."
SOURCE: CHAMPIONI