WANAFUNZI WENYE VIPAJI KUTOKA KENYA WATEMBELEA GLOBAL PUBLISHERS LTD
MHARIRI MTENDAJI WA GLOBAL PUBLISHERS LTD, SALEH ALLY (WA PILI KULIA), AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI HAO PAMOJA NA BAADHI YA VIONGOZI WAO. |
Wanafunzi
wenye vipaji mbalimbali kutoka nchini Kenya, leo wametembelea ofisi za
uchapishaji magazeti za Global Publishers Ltd eneo la Bamaga jijini Dar
es Salaam.
Wanafunzi
hao waliongozwa na Ofisa Mawasiliano wa kampuni ya Africa Nasaha
Production ya nchini Kenya, Oscar Njeru walijifunza mambo kadhaa ya
uandaaji wa magazeti ya Championi, Ijumaa na mengineyo.
Lakini
pia walijifunza namna kazi ya utafutaji habari, zinavyopandishwa
mitandaoni na pia kazi zinazofanywa na Global TV online, runinga ya
mtandaoni inayofanya vizuri zaidi kipindi hiki.