WAFANYABIASHARA KUKUTANA NA MAWAZIRI MJINI DODOMA.
Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango pamoja na Waziri wa Biashara na
Viwanda, Charles Mwijage wanatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na
wafanyabishara Aprili 11,2017 mjini Dodoma kwa lengo la kusikiliza
changamoto zao ili zitafutiwe ufumbuzi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika wiki ya Kongamano la Biashara la Ufaransa na Tanzania, Mwenyekiti wa TPSF Godfrey Simbeye alisema Rais John Magufuli amesikia malalamiko ya wafanyabiashara na kwamba mkutano huo utasaidia kupata suluhu ya changamoto zinazowakabili wafanyabiashara.
Hata hivyo, Simbeye alieleza kusikitishwa kwake na mwitio mdogo wa Kampuni za Kitanzania katika kongamano hilo lililokutanisha kampuni arobaini kutoka nchini Ufaransa, na kusema kuwa zisizohudhuria zimekosa fursa nyingi za kibishara.