AKATWA MKONO KWA MADAI YA SHILINGI LAKI TATU

Picha ya Mwita Magige44 Mkazi wa kijiji cha Keisangora kata ya Nyamwaga Wilayani Tarime Mkoani Mara akiwa na majeraha baada ya kukatwa Mkono wake wa kushoto kwa kile kilichodaiwa kuwa anadaiwa shilingi laki tatu baada ya kukamatiwa Ngombe wake Wanne.



Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina  la Mwita Magige Mkazi wa kijiji cha Keisangora Kata ya Nyamwaga Wilayani Tarime mkoani Mara amekatwana panga mkono wake wa kushoto na kudondoka kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa anadaiwa shilingi Laki tatu baada ya kukamatiwa  Ng’ombe Wake Wanne ambao walikuwa wanachungwa na Mke wake.



 



Akiongea na Cleo24 News Mwita Magige amesema kuwa akiwa Safarini alipigiwa simu kuwa Mifugo yake imekamatwa na ndipo alirejea Nyumbani Kwake na kwenda Eneo la Tukio na kuambiwa na Mwenyekiti wa kijijhi hicho kuwa anadaiwa shilingi laki tatu na badae yowe ilipigwa na ndipo kijana mmoja aliyefaamika kwa jina la Piter Chacha  kwa jina maarufu Bubu alimkata mkono wa kushoto na kuninginia.



 



Nilipofika maeneo ya Mifugo yangu ilipokuwa niliuliza mwenyekiti kuwa Nani ananidai hakuna ambaye alijitokeza na ndipo yowe ilipigwa na kijana mmoja maarufu kwa jina la Bubu alikuja na panga na kunikata nisingweka mkono angenikata kichwa alisema Magige.



Nyangoto Mwita ni Mke wake na Mwita Magige ambae amekatwa mkono huo pia ni shuhuda wa tukio hilo na hapa alisema kuwa akichunga mifugo hiyo alinyanganywa na kupelekwa ili mmewe aweze kulipa kiasi cha shilingi laki tatu.

Powered by Blogger.