VIATU VYEUSI VYA DYABALA ALIYEIUA BARCELONA VYAZUA GUMZO
Mshambuliaji Muargentina, Paulo Dybala
ndiye aliyepiga bao mbili wakati Juventus ikiitwanga Barcelona kwa mabao
3-0 katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tayari sasa gumzo limehamia katika viatu vyeusi ambavyo anavaa mchezaji huyo.
Swali limekuwa kwa mini anavaa viatu vyeusi tupu vikiwa na nembo yake binafsi?
Wapo ambao wameanza kuhusisha viatu hivyo na imani za kishirikina lakini hawaendi moja kwa moja katika suala hilo.
Lakini mjadala wa mitandaoni kwa
Kiitaliano, unaonyesha Dyabala ni mtu wa dini sana kwa kuwa makuzi yake
ni kutoka katika familia ya Kikristo, iliyoshiba imani ya dini hiyo.
Lakini baadhi ya vijana, wanaamini
Dyabala ni mtu anayehusika na nguvu za giza na ndiyo maana anaamini sana
vitu vyenye range nyeusi. Yeye amekuwa kimya na hajalizungumzia hilo.
NEMBO YA DYABALA |