UMOJA WA KIZAZI CHA KUHOJI TANZANIA WALIA NA VITENDO VYA UTEKAJI, UPOTEAJI NA MAUAJI YA RAIA.

 Na James Salvatory, BMG Dar
Umoja wa Kizazi  cha Kuhoji Tanzania (UTG), umeliomba jeshi la polisi kutangaza oparesheni maalumu ya kukomesha vitendo vya utekaji, upoteaji na mauaji ya raia nchini sambamba na kutoa taarifa ya mwenendo wa uchunguzi katika suala la kupotea kwa Ben Saanane.

Hayo yamesemwa leo jijini  Dar es salaam na mwenyekiti wa taasisi ya UTG Godlisten Malisa   alipokuwa akizungumza na vyombo  vya habari ikiwa ni mwendelezo wa harakati za umoja huo kushinikiza kupatikana kwa katibu mkuu wa taasisi hiyo  Ben Saanane ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha tangu mwezi november mwaka jana ambaye mpaka  sasa haijulikani alipo.

Amesema  kuwa kutokana na vitendo hivyo, UTG imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi) kwa tume ya haki za binadamu na utawala bora  ambayo kikatiba ina mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.

 Ameongeza kuwa kutokana na vitendo hivyo,UTG imechukua hatua mbali mbali ikiwemo kuwasilisha malalamiko rasmi (ya maandishi)kwa tume ya haki za binadamu na utawala bora  ambayo kikatiba ina.mamlaka ya kusikiliza mashauri yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu na utawala bora.
Kwa upande wao Agripina Saanane na Erasto  Saanane ni ndugu zake na Ben Saanane wao wameshukuru jitihada za watu mbalimbali  ikiwemo wandishi wa habari, wambunge wananchi katika kuhakikisha kaka yao anapatikana.
Katika hatua nyingine UTG) imeliomba bunge la Jamuhuri ya mMuungano wa Tanzania kujadili hoja kuhusu kudorora hali ya  usalama nchini kufuatia matukio ya kupotea, kutekwa na kuuawa kwa baadhi ya watanzania katika maeneo mbalimbali nchini huku ikitoa pole kwa jeshi la polisi na familia za askari wanane waliopoteza maisha wilayani Kibiti mkoa wa Pwani baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Powered by Blogger.