TOP 10: Watu waliopata mafanikio makubwa duniani wakiwa chini ya miaka 15

Kwa mifano mbalimbali ambayo imekuwa ikituzunguka, wengi tunaamini kuwa mafanikio ya mtu hayawezi kupatikana mpaka mtu afikishe umri fulani lakini kuna mifano mingine mingi ambayo inathibitisha kupata mafanikio katika maisha haitegemei umri wa mtu.
Leo nimekutana na list ya watu 10 duniani ambao wamepata mafanikio makubwa wakiwa chini ya umri wa miaka 15.
1: Gregory Smith
Ni mmoja kati ya watu walioweza kuthibitisha mafanikio hayahusiani na umri wa mtu baada ya kutunukiwa tuzo ya Amani ya Nobel ‘Nobel Peace Prize’ akiwa na umri wa miaka 12. Gregory alijua kusoma akiwa na umri wa miaka miwili na kujiunga Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 10. Sasa Gregory ni kiongozi wa wanasheria duniani.

2: Akrit Jaswal
Akiwa na miaka saba, Akrit alipata umaarufu mkubwa baada ya kufanikiwa kumfanyia upasuaji rafiki yake aliyeungua moto mkononi na vidole kushikana. Alipofikisha miaka 12 alipata nafasi katika Chuo Kikuu cha India ambako alisomea udaktari na mwaka 2011 alipata nafasi ya kufanya mahojiano na mtangazaji mashuhuri wa Marekani Oprah Winfrey katika segment ya ‘Little genious’.

3: Cleopatra Strantan
Cleopatra anajulikana zaidi kama mwanamuziki mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo ya MTV ambapo akiwa na umri wa miaka 3 aliweza kufanya onyesho live kwa muda wa saa 2 mfululizo mbele ya mamilioni ya mashabiki. Aliweka rekodi nyingine ya kuwa mwanamuziki mdogo kutoa album iliyofanya vizuri sokoni.

4: Kim Ung-Young
Guinness Book of Records inamtambua kwa kushika rekodi ya kuwa mtu mwenye IQ kubwa zaidi duniani kwa mwaka 1995. Akiwa na umri wa miaka minne, Kim Ung-Young alikuwa anaweza kuongea lugha za Kikorea, Kijapan, Kijerumani na Kiingereza na alipofikisha umri wa miaka 17 aliaajiriwa na Taasisi ya Mambo ya Anga ya Marekani ‘NASA’.

5: Fabiano Luigi Caruana
Mwaka 2014 Fabiano alitajwa kama Mchezaji Bora wa Chess kuwahi kutokea duniani ambapo akiwa na umri wa miaka 14 alishinda tuzo yake ya kwanza na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kwa level ya Grandmaster.

6: Aelita Andre 
Ni mchoraji wa picha ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya kuchora picha iliyouzwa kwa mamilioni ya pesa akiwa na umri wa miaka miwili. Mwaka 2011 akiwa na umri wa miaka minne alifanya maonyesho katika jumba maarufu la sanaa jijini New York akiwa mchoraji pekee.

7: Michael Kevin Kearny 
Mwaka 2008 Michael Kevin alishinda Dollar milioni 1 kwenye show iliyoitwa Who wants to be a Millionaire baada ya kujibu maswali magumu ya Sayansi na kuibuka mshindi. Kevin alianza kuongea akiwa na umri wa miezi minne na alihitimu masomo ya Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 10.

8: Willie Mosconi
Akiwa na umri miaka 6 Willie Mosconi alikuwa mchezaji mahiri wa Pool Table na aliweza kupata mafanikio mbalimbali kupitia mchezo huo na aliwahi kushinda World Straight Pool Championship kwa miaka 15 mfululizo.

9: Elaina Smith
Aliweka rekodi ya kuwa mtangazaji mdogo zaidi kuwahi kutokea ambapo alianzisha Show yake ya kutoa ushauri akiwa na umri wa miaka 7. Mwaka 2016 alishinda tuzo ya Mwanahabari Bora wa Kike ‘Gracie Award’. Kwa sasa Elaina Smith ni mtangazaji wa show ya asubuhi katika radio maarufu mjini Florida, Marekani.

10: Saul Aaron Kripke
Ni miongoni mwa watu wanaothibitisha kuwa mafanikio hayaletwi na umri ambapo akiwa na umri wa miaka minne aliweza kugundua hesabu za Algebra. Akiwa Secondary Saul Aaron Kripke alialikwa kufundisha katika Chuo Kikuu cha Harvard.
Powered by Blogger.