Mtu mmoja
katika kijiji cha Solwe wilayani Kwimba mkoani Mwanza anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kutokana na imani za
kishirikina.
Tukio
hilo limetokea tarehe 5/04/2017 saa 5 asubuhi ambapo mtu huyo
anayefahamika kwa jina la Kumalija Kondolo Basu anadaiwa kumchoma mke
wake na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na shingoni upande wa
nyuma na kupelekea kifo chake papo hapo.
Inadaiwa
kuwa mtuhumiwa alikuwa akiishi na mkewe nyumbani kwake kijiji cha Bagadu
wilayani Magu lakini hivi karibuni alikwenda kwa wakwe zake wilayani
Kwimba kuwasalimia yeye pamoja na mkewe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa siku ya tukio
mtuhumiwa alibaki nyumbani na mkewe kwani wengine walikuwa wamekwenda
gulioni kwasababu ilikuwa siku ya gulio.
Kwa
mujibu wa Kamanda Msangi, inadaiwa kuwa baada ya mtuhumiwa kuona
wanafamilia hawapo ndipo alimchukua mkewe na kuingia naye ndani na kisha
kutekeleza kitendo hicho.
Amesema
wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo askari
walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa
kumakamata mtuhumiwa.
Amesema
mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa na yupo katika mahojiano na jeshi la
polisi, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani