SI UNAJUA TAMBWE AMEPOTEZA MAKALI YA KUFUNGA? MWAMBUSI HUYU HAPA ANAFAFANUA
Kocha
Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amefunguka kuwa, straika wake,
Mrundi, Amissi Tambwe bado hajawa fiti licha ya kuanza kucheza mechi
kadhaa tangu aliporejea akitokea kwenye majeruhi.
Tambwe
ambaye alikuwa akisumbuliwa na jeraha la enka, wikiendi iliyopita
alirejea uwanjani kucheza dhidi ya Prisons katika mchezo wa Kombe la FA
na kufunga bao moja kwenye ushindi walioupata wa mabao 3-0.
Mwambusi
amesema licha ya Tambwe kufunga bao katika mchezo huo, lakini bado
hajawa fiti kwa asilimia zote kutokana na kukosa baadhi ya vitu vya
kiufundi.
“Tambwe
bado hajawa vizuri kwa asilimia zote licha ya kufunga bao muhimu kwa
timu kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua hapo kabla.
“Lakini taratibu atakuwa fiti na kuisaidia timu kwenye michezo iliyosalia katika michuano tunayoshiriki ambayo yote tunataka kuchukua mataji yake,” alisema