SHUJAA SIMBU ALIVYOREJEA NA MAPOKEZI YAKE KUONGOZWA NA SERIKALI NA WADHAMINI WAKE MULTICHOICE TANZANIA
Balozi maalum wa DStv na Mwanariadha pekee wa Tanzania liyeshiriki mashindano ya London Marathon Alphonce Simbu amerejea nyumbani na kutoa onyo kali kwa wale atakaokabiliana nao kwenye mashindano yajayo ya dunia yatakayofanyika mwezi Agosti jijini London.
Simbu
ambaye alishika nafasi ya tano katika mashindano hayo na kujishindia
kitita cha dola za marekani 10,000 aliwasili katika uwanja wa Ndege wa
kimataifa wa Kilimanjaro na kulakiwa na maafisa mbalimbali akiwemo
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana, Meneja wa
mwanariadha huyo Francis John
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Arusha muda
mfupi baada ya yeye kuwasili Simbu aliwashukuru sana watanzania wote kwa
moyo wao na jinsi walivyomuunga mkono na kumtakia kila la heri katika
mashindano hayo. Amesema alifarijika sana na pia kupata moyo zaidi
alipokuwa akipokea salamu kutoka kwa watanzania kote ndani nan je ya
nchi.
Akizungumzia
mashindano hayo, Simbu amesema yalikuwa na changamoto kama yalivyo
mashindano mengine makubwa ya kimataifa kwani yalishirikisha vigogo
ambao wengi wao wana uzoefu mkubwa katika mashindano mbalimbali na
wengine pia ni washindi wa mashindano ya hapo awali.