RONALDO BAO LA KWANZA ALIPIGIA MANCHESTER, BAO LA 100 KAPIGA MUNICH, AMETUMIA SIKU
Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 100 katika michuano ya Ulaya.
Bao
la 99 na like la 100 amefunga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
hatua ya robo fainali wakati Real Madrid ilipoitwanga Bayern Munich kwa
mabao 2-1, kwao Munich, Ujerumani.
Amefikisha mabao 100 baada ya kutumia siku 4,264 katika maisha yake ya soka la Ulaya.
Mara
ya kwanza kufunga bao la kwanza la Ulaya ilikuwa mwaka 2005, ikiwa
katika hatua za kufuzu wakati Manchester United ilipoitwanga Debrecen
kwa mabao 3-0.
Tokea mwaka 2005, Ronaldo amecheza jumla ya mechi 140.