Mauaji ya Kutisha: POLISI WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI TANZANIA
Askari polisi saba waliokuwa katika
doria kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani
Pwani nchini Tanzania wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa
Aprili 13,2017.
Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa
polisi mkoa wa Pwani.
Taarifa zinasema kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni
kutoka kwenye doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.
Imeelezwa kuwa majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa
kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio,
kisha kutokomea kusikojulikana na kwamba silaha zote walizokuwa nazo
(SMG) zilichukuliwa na watu hao.
Taarifa zaidi tutawaletea...endelea kutembelea CLEO24 NEWS