Rais Magufuli Aagiza TCU kutowachagulia Wanafunzi wa Elimu ya Juu Vyuo
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya Hostel
mpya 20 za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi rasmi wa
Hostel hizo leo Jijini Dar es Salaam. Hostel hizo zilizogharimu takribani sh.
Bilioni 10 zilizotolewa kufuatia ahadi ya Rais Maguful,i ambapo ujenzi wake
umefanya na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) chini ya usimamizi wa Jeshi la
Wananchi Tanzania ambapo linatarajiwa kutumiwa na wanachuo 3840.Kutoka Kulia ni
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa. Makame Mbarawa na Makamu
Mkuu wa Chuo hicho Profesa Rwekaza Mukandara (katikati).
|
Kwa ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam ikitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo mapya ya
Hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo Jijini Dar es Salaam.
|
Na: Lilian Lundo na Beatrice Lyimo
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu
ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.
Agizo
hilo limetolewa leo, Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alipokuwa
akizindua Mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni ahadi
yake aliyoitoa Chuoni hapo Juni, mwaka jana.
“Ninaamini
kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda
wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema
Dkt. Magufuli.
Aliendelea
kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na
sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma
katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana
na vyuo hivyo kutokuwa na sifa.
Aidha,
Rais Magufuli ameuagiza uongozi wa UDSM kutoza wanafunzi gharama ya
shilingi mia tano(500) kama malipo ya makazi ya mabweni hayo kwa siku
badala ya shilingi mia nane(800) inayotozwa kwa mabweni mengine yaliyopo
chuoni hapo.
Alisema
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuwekeza katika elimu hivyo
itahakikisha wanafunzi nchini wananufaika kwa kupata elimu bora kuanzia
shule za msingi hadi vyuo vikuu.
“watanzania
walinichagua ili kutatua changamoto zinazowakabili na hivi ndivyo
ninavyofanya kutatua changamoto hizo” alisema Rais Magufuli.
Naye,
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako
amempongeza Rais Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya
ujenzi wa mabweni hayo ambao kwa kiasi kikubwa yatatatua changamoto ya
makazi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa chuo hicho.
Prof. Ndalichako amesema kuwa mabweni hayo yamejengwa kwa kipindi cha miezi 8 ambayo yatachukua wanafunzi 3840.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Kikuu cha Dar es Salaam Prof.
Rwekaza Mukandala ametoa rai kwa wanafunzi wa chuo hicho kuhakikisha
wanaimarisha usalama katika maeneo ya mabweni hayo na kulinda miundo
mbinu yote iliyoweka.
“Ni
lazima mzingatie matumizi sahihi ya kila kifaa kilichofungwa katika
majengo haya, majengo haya ni mapya na yamejengwa kwa gharama kubwa kwa
lengo la kutusaidia kuondokana na changamato iliyotukabili kwa muda
mrefu,” alisema Prof. Mukangala.
Wakati
huohuo Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba
za makazi magomeni “QUARTERS”, mradi ambao kwa asilimia kubwa unawagusa
watanzania wa hali ya chini.
Aidha
Rais Magufuli ameendelea kusisitiza juu ya ahadi aliyoitoa kwa wakazi
644 waliokuwa wakiishi maeneo hayo kupewa nyumba ambapo wataishi bure
kwa muda wa miaka mitano.
Pia,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo (TBA) Msanifu Majengo Elvis
Mwakalinga amesema ujenzi wa mradi huo umezingatia miundombinu yote
iliyohitajika ambapo itakuwa na sehemu za makazi, biashara, maegesho ya
magari na bustani ya kupumzikia.
Ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo ujenzi wake ulianza rasmi Octoba mwaka jana.