MWANAUME AJIUA KWA KUJINYONGA KWA KAMBA YA KATANI MWANZA
****Mtu mmoja amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani wilayani nyamagana.
****Mtu
mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana akiwa na
pombe iliyohifadhiwa kwenye vifungashio vya plastiki almaarufu viroba
pakiti 103 wilayani ilemela.
Kwamba
tarehe 23.04.2017 majira ya 18:45hrs jioni katika mtaa wa mkuyuni
sokoni kata ya mkuyuni wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza, mtu
mmoja mwanamume aliyefahamika kwa jina la faraja anselem miaka 31, mkazi
wa mtaa wa mkuyuni sokoni, alikutwa akiwa amejinyonga chumbani kwake
hadi kufariki dunia kwa kutumia kamba ya katani aliyokuwa ameifunga
kwenye paa la chumba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Inasemekana
kuwa taraehe tajwa hapo juu marehemu alibaki mwenyewe nyumbani, aidha
inadaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo marehemu alionekana akiingia
chumbani kwake kisha akafunga mlango ndipo baada ya muda kupita watoto
waliokuwa wakicheza maeneo hayo waliona miguu ikining’inia dirishani
ndipo walitoa taarifa kwa wazazi wao.
Majirani
baada ya kuona tukio hilo walitoa taarifa polisi, ambapo askari
walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kuukuta mwili wa
marehemu ukining’inia mahali hapo, mwili wa marehemu umehifadhiwa
hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi
ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Aidha upelezi kuhusiana na kifo hicho bado unaendelea.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa
wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza, akiwaomba kuwa pale
watakapoona mtu amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu hadi
inapelekea kuweza kufanya kitu kisicho cha kawaida cha kuweza kujidhuru
yeye mwenyewe au watu wengine, wamfikishe kwa wataalamu wa ushauri
nasaha ili waweze kumshauri na kumwaondoa katika hali hiyo ya msongo wa
mawazo na kisha kurudi katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na
maisha.
Katika tukio la pili,
Kwamba
tarehe 23.04.2017 majira ya saa 14:33hrs katika mtaa wa kiloleli kata
ya nyamanoro wilaya ya ilemela jiji na mkoa wa mwanza, askari wakiwa
doria na misako walifanikiwa kumkamata mtu aliyefahamika kwa jina la
donatus sebastina miaka 16, mkazi wa kiloleli akiwa na pombe iliyeowekwa
kwenye vifunganishio vya plastiki almaarufu viroba aina ya empire
pakiti 103, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Awali
askari wakiwa kwenye doria na misako walipokea taarifa kutoka kwa
wasiri kwamba maeneo tajwa hapo juu yupo mtu anayefanya biashara ya
kuuza pombe ya viroba kwa siri, kutokana na taarifa hizo askari
walifanya upelelezi wa kimyakimya huku wakiendelea na doria ndipo baada
ya muda waliweza kufahamu mahali anapoishi mtuhumiwa na kufanikiwa
kumkamata akaiwa na pakiti 103 za pombe iliyohifadhiwa kwenye
vifungashio vya plastiki almaarufu viroba aina ya empire.
Mtuhumiwa
yupo katika mahojiano na polisi, pindi uchunguzi ukikamilika
atafikishwa mahakani, aidha upeleezi na misako ya kuwatafuta watu
wengine wanaojihusisha na biashara hiyo ya pombe za viroba bado
unaendelea.
Kamanda
wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa
wito kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuendelea kutoa
taarifa mapema kwa jeshi la polisi ili watu wanaojihusisha na biashari
hiyo ya pombe za viroba waweze kukamatwa na kifikishwa katika vyombo vya
sheria.
Imetolewa na:
Dcp: Ahmed Msangi.
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza