MASHINDANO YA MEI MOSI KITAIFA YAZINDULIWA MJINI MOSHI- TAZAMA PICHA


Timu ya Watumishi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiingia uwanjani kwa maandamano wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika mjini Moshi.
Timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiingia uwanjani .
Timu ya Wizara ya Uchukuzi wakingia uwanjani.
Timu za Mashirika na Taasisi mbalimbali wakiwa wamebeba mabango wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi yanayofanyika kitaifa mjini Moshi.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Awadi Safari akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliodfanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Mei Mosi Kitaifa ,Joyce Benjamini akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa mashindano hayo ,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa hotuba ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba (aliyevaa suti) akiongozana na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Mei Mosi kitaifa ,Joyce Benjamin kwa ajili ya ukaguzi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo.
Mwamuzi wa Kike ,Salma akimtamburisha Mkuu wa wilaya timu mbalimbali zilizopo pamoja na kumkaribisha kwa ajili ya ukaguzi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa timu ya Geita Gold Mining.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akisalimiana na wachezaji wa Netiboli wa timu ya RAS Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mei Mosi kitaifa yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Timu ya soka ya Geita Gold Mining wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya RAS -Kilimanjaro .
Timu ya soka ya RAS -Kilimanjaro kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo wake dhidi ya Geita Gold Mining ,mchezo ulimalizika kwa timu ya RAS-Kilimanjaro kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Kikosi cha timu ya TPDC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake dhidi ya timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Kikosi cha timu ya Halmashari ya wilaya ya Hai kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wake dhidi ya TPDC mchezo uliomalizika kwa TPDC kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.
Mshambuliaji Tumaini Masue wa timu ya Chuo Kiku cha Ushirika Moshi,akijaribu kumpita mlinzi wa timu ya RAS -Kilimanjaro mchezo ambao timu ya Ushirika ilichomoza na ushindi wa bao 2-1.
Wachezaji wa timu ya TPDC na Halmashauri ya wilaya ya Hai,wakichuana vikali .
Mchezo mwingine ulikuwa ni netiboli ambapo ,timu zimekuwa zikichuana vikali kuwania umalkia wa mchezo huo.
Timu za TPDC na MUHAS zikimenyana katika mchezo wa kuvuta Kamba ,mchezo ulimalizika kwa TPDC kushinda mhezo huo baada ya kuwavuta wenzao kwa awamu mbili.
****
KAMATI ya Mashindano ya Mei Mosi ,imeonya timu za Mashirika kutumia wanamichezo wasio watumishi (Watumishi Bandia ) katika mashindano hayo huku ikitangaza kutoa adhabu kali kwa taasisi ama mashirika yatakayobainika kuwatumia wachezaji hao.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo ambayo hufanyika katikamkoa ambao siku kuu ya Wanyakazi Duniani hufanyika kitaifa, timu zitakazo bainika kufanya udanganyifu zitafikwa na rungu la kufungiwa mwaka mmoja kutoshiriki mashindano hayo pamoja na faini ya kiasi cha sh 500,000.
Mbali na adhabu hiyo kwa timu iliyofanya udanganyifu ,pia viongoz wa timu husika watafungiwa kwa muda wa miaka miwili kushiriki mashindano ya Mei mosi ,adhabu itakayoenda sambamba na nakala ya barua kwa waajili wa viongozi hao ya kuonesha namna watumishi hao si waaminifu.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Mashindano hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCu) baada ya kuzinduliwa jana ,Hawad Safari alisema ili kutoa uhakiki kamati imetoa maelekezo kwa wanamichezo wafike na vitamburisho vya kazi,Fomu inayoonesha mshahara pamoja na kadi ya bima ya afya.
Alisema mashindano hayo yanahusisha timu kutoka katika mashirikisho manne ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Uma (SHIMUTA),Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI ) ,BAMATA na Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA).
Safari alisema hadi sasa jumla ya timu 14 kutoka taasisi na mashirika mbalilimbali zimewasili mjini hapa kwa ajili ya kushindana katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,Netiboli,Kuvuta kamba ,Mbio za baiskeli ,Marathoni pamoja na michezo ya jadi kama Bao ,Drafti na Karata.
Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mashindano hayo uliotanguliwa na maandamano kwa timu shiriki,Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba alisema zipo taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa taasisi na mashirika wamezuia kushiriki michezo hiyo licha ya kwamba timu zao zilikwisha fanya maandalizi.
“Nivitake vyama vyama vya wafanyakazi kufuatilia suala hili ,kwa nini wafanyakazi hawashiriki katika michezo hasa hii ya Mei Mosi Kitaifa ….nchi yetu imekuwa haipigi hatua kwenye eneo hili ni kwa sababu ya viongozi hawa wasiopenda michezo mahala pa kazi”alisema Warioba.
Awali akitoa hotuba yake Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano hayo Joyce Benjamini alisema Mashindano hayo yamelenga kuongeza ushirikiano mwema kwa wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi huku akitoa rai kwa viongozi kutenga bajeti kwa ajili ya mashindano hayo.
Timu zinazo shiriki mashindano hayo ni pamoja na Wizara ya Uchukuzi,Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makao –CDA Dodoma,Ofisi ya Rais Ikulu,Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Timu nyingine ni Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU),Halimashauri ya wilaya ya Hai,Halmahauri ya wilaya ya Moshi ,Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Ofisi ya katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Geita Gold Mining,Mamlaka ya Hifadhi ya taifa ya Ngorongoro na TAMISEMI.
Katika michezo ya awali timu ya soka ya TPDC ilifanikiwa kuchomoza na ushindi baada ya kuiadhibu timu ya Halmashauri ya wilaya ya Hai kwa bao moja kwa sifuri huku timu ya Chuo Kikuu cha Ushirika ikitakata mbele ya timu ya Ras –Kilimanjaro kwa jumla ya ba 2 kwa 1.
Powered by Blogger.