Na James Salvatory, BMG
Watanzania wametakiwa kuzitumia vyema fursa za kifedha hapa nchini ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa benki ya Africa (BOA BANK)
Wasia Mushi, wakati akizungumza na wanahabari katika hafla fupi ya benki
hiyo ya kutimiza miaka 13 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini mwaka
2007.
Alisema kama wananchi watazitumia fursa za kifedha ikiwemo kupata mikopo
na kuitumia katika malengo walioyakusudia mikopo hiyo itawasaidia
wananchi hao kufanikiwa hasa katika biashara na hatimaye kurejesha
mikopo yao bila kupata hasara katika biashara zao.
Benki hiyo imekuza mtaji wake kutoka bilion 3 mwaka 2007 mpaka kufikia
bilioni 37 mwaka 2017 na imewekeza katika nchi 18 ikiwemo nchi ukanda wa
afrika ya kati,ukanda wa afrika mashariki na bahari ya hindi ikiwemo
Tanzania ambapo kwa Tanzanja benki hiyo ina matawi 27 huku matawi 14
yakiwa jijjni Dar es salaam na 13 mikoani na ina wateja wapatao laki
moja na arobaini huku amana yake ikiwa ni bilioni 325