MAPEMAAAAA...MBAO FC WAELEZA WATAKAVYOING'OA YANGA NA KUTINGA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO
Kikosi cha Mbao FC cha mkoani Mwanza kina imani ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho kwa kuing'oa na kuivua ubingwa Yanga.
Mbao
FC wanajiamini kutokana na safu nzuri ya ushambuliaji, lakini wameandaa
safu yao ya ulinzi kikamilifu kuwadhibiti Simon Msuva na Amissi Tambwe,
kuhakikisha hawapati nafasi ya kufunga.
Mbao
inatarajia kukutana na Yanga Jumapili katika Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA ambapo hadi
sasa ni timu nne tu ndizo zilizobakia.
Msemaji
wa Mbao FC, Chrisant Malinzi, amesema kuwa, walikuwa na hamu kubwa ya
kukutana na Yanga kwenye FA na kudai kuwa wameiandaa ipasavyo safu yao
ya ulinzi kuhakikisha wanatoa upinzani mkubwa kwa Msuva na Tambwe ili
wasipate nafasi ya kufunga kwa kuwa wanahitaji kutinga fainali.
“Tulianza
mipango yetu siku nyingi ya kujiandaa katika michuano ya Kombe la FA na
tulikuwa tukisubiria tu timu ya kupangwa nayo, tulikuwa na kiu ya
kucheza na Yanga, kwani tupo tayari kwa mchezo huo na wala hatuhofii
safu ya ushambuliaji ya Yanga kwani na sisi tuna safu nzuri ya ulinzi ya
kuweza kuwazuia Msuva na Tambwe, tumejipanga vyema kuhakikisha tunapata
nafasi ya kuingia fainali.
“Kikosi
chetu kipo vizuri na hadi tunafikia hapa ni juhudi za wachezaji hivyo
nina imani tutafanikiwa kufanya vyema na hatimaye kuingia fainali kwani
lengo letu ni kuona tunafanikiwa kutwaa taji ili kuwakilisha nchi
kimataifa,” alisema Malinzi.
SOURCE: CHAMPIONI