GENK YA SAMATTA YAAMBULIA SARE YA 1-1 YEYE AKICHEZA DAKIKA 90



KRC Genk imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Eupen katika mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji hatua ya Play off.

Genk iko Kundi B katika hatua hiyo na Mtanzania Mbwana Samatta amecheza kwa dakika zote 90 za mechi hiyo.

Bao la Genk limefungwa na Ruslan Malinovsky katika dakika ya 20 na likadumu hadi mapumziko.


Wenyeji walisawazisha katika dakika ya 51 kupitia Luis Garcia kwa mkwaju wa penalti.
Powered by Blogger.