DE GEA SAFARI YA KUREJEA MADRID "IMEKWIVA", ALIWEKA SOKONI JUMBA LAKE LA KIFAHARI
Dalili zote sasa kwamba kipa, David De Gea wa man United atarejea Hispania na kujiunga na vigogo, Real Madrid.
Hii
inatokana na uamuzi wa kips huyo aliyejiunga na Man United mwaka 2011
akitokea Atletico Madrid kuliweka sokoni jumba lake la kifahari
analoishi.
De Gea ametangaza kuliuza jumba hilo lenye thamani ya pauni million 3.85.
Kwa
zaidi ya mwaka mmoja sasa, Madrid imekuwa ikipambana kumpata De Gea
ambaye anaonekana ndiye kipa tegemeo wa timu ya taifa ya Hispania.