BAADA YA KICHUYA KUPATA HABARI TOTO NI KIBOKO YA SIMBA, HII NDIYO KAULI YAKE...
Kiungo mshambuliaji
wa Simba, Shiza Kichuya, amesema mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Toto
Africans itakuwa ngumu lakini nia ni kupata ushindi na kuvuruga rekodi
ya Toto kutofungwa na Simba ndani ya miaka saba kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba.
“Nimesikia Simba
haijawahi kuifunga Toto kwa miaka saba katika Uwanja wa Kirumba,
wachezaji kwa pamoja tumedhamiria kushinda mchezo huo.
“Yawezekana mchezo huo ukawa balaa kwa kuwa tumejipanga kupata matokeo mazuri kwa kuibuka na pointi tatu."
Toto ni moja ya
timu zimekuwa zikiisumbua sana Simba na mara nyingi zimekuwa zikikutana
katika mechi ya mzunguko wa pili ambayo huchezwa jijini Mwanza.
Mara nyingi, wakati zinakutana, Simba huwa inawania kubeba ubingwa na Toto ikipambana kujikomboa kuteremka daraja.