WATU 9 WAJERUHIWA VURUGU ZA MGAMBO NA MACHINGA MWANZA
Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa
wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana,
mkoani Mwanza.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema
kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya
saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo
askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na
dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa.
Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya
miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara
pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia
wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo
katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza
kwenda shinyanga.
Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari
walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa
wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi
utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.
Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.