RAIS MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGEVITA NGERENGERE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 06 Machi, 2017 amezindua
uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere uliopo Mkoani Morogoro,
uliofanyiwa ukarabati mkubwa baada ya miundombinu ya uwa
nja uliojengwa tangu mwaka 1970 kuharibika.
nja uliojengwa tangu mwaka 1970 kuharibika.
Sherehe ya uzinduzi wa uwanja huo imefanyika uwanjani hapo na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein
Ali Mwinyi, Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Viongozi
wa vyombo vya ulinzi na usalama na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania wastaafu.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amesema
ukarabati wa uwanja huo ulioanza tarehe 15 Julai, 2013 umegharimu
Shilingi Bilioni 137 na Milioni 631 ikiwa ni ufadhili wa Serikali ya
China na umehusisha kujenga upya njia ya kuruka na kutua ndege yenye
urefu wa mita 3,000 upana wa mita 45 na unene wa sentimeta 45 pamoja na
maegesho ya ndege za kivita na ndege za abiria.
Jenerali Mabeyo ameongeza kuwa uwanja huo ni miongoni mwa viwanja bora
zaidi duniani kwa sasa na una uwezo wa kutumiwa na ndege za aina zote
zilizo chini ya Boeing 777 huku akibainisha kuwa pamoja na ndege za
kivita pia unaweza kutumiwa na ndege za kawaida za abiria kwa dharula.
Nae Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing amesema kujengwa
kwa uwanja huo kumeimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya
Tanzania na China na amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuendeleza
uhusiano huo.
Pamoja na kuzindua uwanja huo, Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia maonesho
ya ndege za kivita zilizorushwa kwa mbinu mbalimbali za kivita, kutoa
heshima na kutua katika uwanja huo.
Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kazi kubwa linayofanya na pia
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na Serikali
yake kwa msaada mkubwa iliyoutoa kujenga uwanja huo.
“Mhe. Balozi Lu Youqing naomba unipelekee shukrani zangu za dhati Mhe.
Rais wa China kwa kutoa msaada huu mkubwa wa kujenga uwanja wa ndegevita
wa Ngerengere, najua China imetusaidia kujenga Reli ya TAZARA, Kiwanda
cha Urafiki na Uwanja wa Mpira, hii yote inathibitisha uhusiano wetu
mzuri, urafiki na undugu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli ameahidi kujenga barabara ya lami ya
kuunganisha Kamandi ya Jeshi la anga ya Ngerengere na barabara kuu ya
Dar es Salaam – Morogoro.