Uhakiki wa wastaafu
wanaolipwa Pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango wakiendelea na uhakiki katika
viwanja vya Karimjee leo Jijini Dar es
Salaam.Zoezi hili linafanyika kwa wiki nzima kuanzia tarehe 6-10 Machi kwa
wastaafu walio Dar es Salaam.
Picha/Habari na Daudi Manongi
Mkaguzi
Mkuu wa Ndani wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito kwa wastaafu wanaolipwa
Pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango ambao ni wagonjwa na hawawezi kufika
katika viwanja vya Karimjee na Mwalimu Nyerere(Sabasaba) kwa ajili ya uhakiki
wa nyaraka zao kutoa namba za simu na majina yao ili waweze kuhakikiwa pale
walipo kama ni Hospitali au nyumbani.
Bw.Mohamed
Mtonga ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa
habari juu ya zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa pensheni na
Wizara ya Fedha na Mipango linalofanyika katika Jiji la Dar es Salaam kuanzia
leo tarehe 6-10 Machi.
“Kwa
sasa ninavyozungumza zoezi hili liko kwenye hatua ya mwisho katika Mkoa wa Dar
es Salaam,Zoezi hili lilianza Mkoa wa Pwani na tumelifanya nchi nzima na
limefanyika kwa ufanisi mkubwa sana na wastaafu wengi wamejitokeza na kama
mnavyoona zoezi limekuwa likiendelea kwa utaratibu mzuri sana”,Aliongeza
Bw.Mtonga.
Mtonga
amesema wastaafu hao wengi ni watumishi wa Serikali ambao walifanya kazi kabla
ya mwaka 1999 ambapo walikuwa hawapo katika mifuko ya pensheni ndio ambao
wanalipwa pensheni na Serikali wakiwemo watumishi wa vyombo vya ulinzi na
usalama.
Aidha
amesema lengo kubwa la kuhakiki wastaafu hao ni kuboresha daftari la wastaafu
ili kusaidia kujua ni kiasi gani cha wastaafu wapo katika kumbukumbu ya daftari
la pensheni na kusisitiza wastafu ambao hawatajitokeza watafutwa katika daftari
hilo.
Ukaguzi
huu kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 na ukaanza tena mwezi Octoba mwaka
2016.
|