WABUNGE WAPAMBA KONGAMANO LA MUZIKI JIJINI DAR ES SALAAM.
Mbunge
na Katibu Mkuu Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania
(UWT), Amina Nassoro Makulagi (kulia), akizungumza katika Kongamano la
Siku moja la wadau wa muziki nchini lililoandaliwa na Tanzania Music
Foundation (TMF) na kufanyika Ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii,
Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mtaalamu
wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo na
Rais wa TMF, Dk.Donald Kissanga.
Mbunge, Halima Bulembo, akizungumza kwenye kongamano hilo.
Mbunge, Kiteto Zawadi Koshuma akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Rais
wa TMF, Dk.Donald Kissanga, akizungumza katika kongamano hilo, Kutoka
kulia ni mtoa mada, Dk. Baraka Kanyabuhinya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Rais wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania (Chamruta),
Dk.Salim Mwinyi na Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo.
Mwezeshaji katika kongamano hilo, Dk.Baraka Kanyabuhinya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akizungumza.
Rais wa Chama cha Muziki wa Rhumba Tanzania (Chamruta), Dk.Salim Mwinyi akizungumza.
Mchungaji Simon Mkologo kutoka nchini Malawi akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi wa Polisi Ezekiel Kyogo akizungumza machache katika kongamano hilo.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania, Stella Joel akiongoza kongamano hilo.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa
Benki ya Equity Tanzania LTD, Janety Zoya (kushoto), akizungumzia kazi
mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo na masuala ya kifedha. Kulia ni
Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mwenge, Godfrey Kiama.
Wanamuziki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Wasanii ndani ya ukumbi.
Wanamuziki wakiwa katika kongamano.
Muonekano wa ukumbi huo.
Hapa ni mserebuko kitambaa cheupe juu.
Mwanamuzi mkongwe na muimbaji wa nyimbo za injili Dk. Makassy alikuwepo kwenye kongamano hilo.
Mwanamuziki, Kikumbi Mwanza Mpango (King Kiki), naye alikuwepo kwenye kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imeombwa kuangalia kwa karibu
mapungufu ya adhabu ya makosa ya wizi wa kazi za wasanii ili kuweza
kusaidia kukua kwa pato la taifa linalopotea kutokana na wizi huo.
Hayo yamesemwa na Mtaalamu wa Sheria kutoka Jeshi la Polisi Dk. Mkaguzi
wa Polisi Ezekiel Kyogo katika kongamano la siku moja lililowakutanisha
wadau wa muziki wakiwemo wa muziki wa injili lililofanyika Ukumbi wa
Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema kongamano hilo lina lengo la kuwajengea uelewa wasanii wa
muziki juu ya kazi zao, hususani changamoto na suluhu za kazi za Sanaa
nchini.
Kyogo alisema kazi za Sanaa ni mali lakini zimekosa ulinzi pamoja na
jitihada zilizopo bado nguvu zaidi inahitajika kama vile kuangalia
Sheria ya haki miliki ya mwaka 1966 na 1999.
Alisema jitihada zaidi zinatakiwa kwa ajili ya kuongeza nguvu ili
tufike mahali ambapo wasanii wataweza kunufaika na kazi zao ili na wao
waweze kulipa kodi na serikali kupata mapato yake.
Kyogo alishauri sheria ya makosa ya wizi wa kazi za wasanii ibadilishwe
iwe katika makosa ya jinai na isimamiwe na jeshi la polisi kama
inavyosimamia makosa mengine tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kazi
hiyo inafanywa na wasanii wenyewe na kukosa nguvu ya ufatiliaji
wahalifu.
Aliongeza kuwa wasanii wamekosa ubunifu na watu wamekata tamaa na
kujiingiza katika wimbi la dawa za kulevya lakini wakipatiwa elimu na
kujengewa mazingira mazuri ya uuzaji wa kazi za sanaa waifanyayo
itawasaidia na kutoingia katika tamaa ya kupata fedha kwa njia
zisizostahili.
Alisema kuwepo kwa mapungufu ya adhabu haipunguzi uhalifu kwani
wasimamizi wa sheria wanatakiwa kuwa na uwezo zaidi katika sheria hizo
ili kusaidia kutokomeza wizi wa kazi za wasanii.
“Lazima kuwe na sheria ya makosa ya wizi za kazi za wasanii kwani
itasaidia kupunguza wizi na itaongeza kipato na ajira, kwa kuwa muziki
ni mali ya jamii na ni afya na tiba”, alisema Kyogo.
Rais wa Tanzania Music Foundation (TMF) Dk. Donald Kassanga aliongeza
kuwa lengo kubwa la kongamano hilo ni kuhakikisha serikali inatengeneza
mazingira bora katika tasnia nzima ya muziki jambo litakalosaidia
kuongeza pato la taifa.
“Watu wamekuwa wakiiba kazi za wasanii na kama TMF tunalaaani na kuomba
serikali kupitia vyombo vya dola kuziba mianya hiyo" alisema Dk.
Kissanga.
Katika hatua nyingine alisema TMF inaungana na Serikali katika mapambano
ya dawa za kulevya nchini kwani waathiri ni pamoja na wanamuziki na
wasanii kwa ujumla.
Mwimbaji wa nyimbo za injili, Faraja Ntaboba, alisema kuwa wasanii
wamekuwa wakiibiwa sana kazi zao wakati wanatumia nguvu kubwa kwa
kuziandaa.
"Tuna amini
endapo Serikali ikisimamia vizuri kwa kushirikiana na TMF wataweza
kulipa kodi sawa sawa na kuendesha kazi vizuri" alisema Ntaboba.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)