UTAFITI KUHUSU WATU WANAOPENDA KUDANGANYA UMRI WAO

Ni kawaida kwa watu kuficha na wakati
mwingine kudanganya umri wao pengine kwa kuhofia kuonekana ama wadogo
sana au wakubwa zaidi katika kundi la watu.
Utafiti uliofanywa unadai unaweza kuendelea kuuficha umri wako na kuwadanganya watu kwa sababu itakusaidia kuishi zaidi.
Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa watu wanaoamini kuwa ni wadogo kiumri
tofauti na kilichopo katika vyeti vyao vya kuzaliwa ni miongoni mwa
kundi la watu wenye uwiano mdogo wa kufa ukilinganisha na ama wanaouhisi
umri wao au wanaojifaya wakubwa kuliko umri wao .
Utafiti umechapishwa na JAMA INTERNAL MEDICINE ONLINE ambao ulikusanya
data kutoka kwa watu 6,489 wenye wastani wa miaka 65.8 ambao wanaelezwa
kujihisi watoto wa chini ya umri wa miaka 10.
Kinachofurahisha zaidi ni kuwa watu wengi kwenye utafiti huo hawakuwa na
hisia na umri wao halisi ambapo wengi walidai kujihisi kama watoto wa
miaka mitatu huku 4.8% walikuwa wanajihisi wakubwa zaidi ya umri wao.