MASHINDANO YA MABALOZI WA MTOTO MFANYAKAZI WA NYUMBANI YAFANA JIJINI MWANZA.
Mgeni rasmi, Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza, Kizito Wambura (kulia), akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika viunga vya shule ya msingi Nyamagana.
#BMGHabari
Wanafunzi wa shule ya msingi
Nyamagana wameibuka washindi kwenye mashindano elimishi kwa klabu za
mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani dhidi ya wakubwa zao kutoka
shule ya sekondari Nyakurunduma, zote za Jijini Mwanza.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na
taasisi ya kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) ya
Jijini Mwanza, yalijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo maigizo, ngonjera
pamoja na mashairi yenye jumbe za kuainisha aina za ukatili
wanaokumbana nao watoto wafanyakazi wa majumbani ikiwemo vipigo,
utumikishwaji na fursa ya kukosa elimu, na kuiasa jamii kuachana na
vitendo hivyo.
"Ukiona mtoto anatendewa ukatili wa
aina yoyote, paza sauti (toa taarifa) sehemu mbalimbali ikiwemo
WoteSawa, polisi kupitia kitengo cha dawati la jinsia, kwa Mwenyekiti wa
Mtaa ama Mtendaji wa Kata". Amesisitiza mgeni rasmi, Wambura.
Naye Mkurugenzi wa taasisi ya
WoteSawa, Angel Benedicto, amebainisha kwamba bado watoto wafanyakazi wa
majumbani wanakabiliwa na vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo
kutumikishwa kwa kuajiriwa ili kutembeza bidhaa mtaani kwa ujira mdogo,
kunyimwa fursa ya kusoma pamoja na vipigo kutoka kwa baadhi ya waajiri
hivyo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu katika jamii ili kuhakikisha
vitendo hivyo vinatokomezwa.
"Lengo ni kupunguza ukatili wa watoto
majumbani, kulinda haki za watoto, kuibua vipaji ikiwemo uchoraji na
uigizaji ili kuvitumia katika kufikisha elimu ya kupambana na ukatili
dhidi ya watoto". Imefafanua sehemu ya risala ya klabu za wanafunzi
mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya msingi
Nyamagana na Nyakurunduma sekondari, iliyosomwa na Neema Christopher.
Shule ya msingi Nyamagana wakifurahia
ushindi wao ambapo igizo wamepata asilimia 93 dhidi ya 92 za Nyamagana
sekondari, Shairi Nyamagana wamepata asilimia 74 dhidi ya 85 za
Nyakurunduma huku Ngonjera Nyamagana wakipata asilimia 91 dhidi ya 77 za
Nyakurunduma. Ushindi wa jumla, shule ya Msingi Nyamagana wamepata
asilimia 86 dhidi ya 85 za Nyakurunduma sekondari.
Mabalozi kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma wakipokea kombe baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo
Pia mabalozi wote wamepatiwa vyeti kwa kujitoa kuwa mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Mabalozi wakipokea vyeti
Mabalozi kutoka shule ya msingi Nyamagana wakionesha makali yao katika ngonjera na mashairi
Mabalozi kutoka Nyakurunduma sekondari wakighani mashairi na ngonjera
Afisa Ustawi wa jamii Jijini Mwanza, Davis Justine (katikari) akitoa matokeo ya mashindano hayo kwa niaba ya majaji wengine
Mkurugenzi wa WoteSawa, Angel Benedicto, akizungumza wakati wa mashindano hayo
Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha, akizungumza kwenye mashindano hayo
Taasisi ya WoteSawa imechora mchhoro huu
katika shule ya Msingi Nyamagana, ukiwa na jumbe mbalimbali ikiwemo
"Mpe elimu siyo kumuajiri kazi za nyumbani" ikiwa ni mwendelezo wa
kufikisha elimu juu ya mapambano dhidi ya ukatili wa mtoto mfanyakazi wa
nyumbani.
Mgeni rasmi akizungumza jambo kwenye mashindano hayo na kuzindua pia mchoro huo
Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani
kutoka shule ya sekondari Nyakunduruma Jijini Mwanza wakiwa na vyeti
vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani
kutoka shule ya shule ya msingi Nyamagana Jijini Mwanza wakiwa na vyeti
vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
Mabalozi wote wakiwa kwenye picha ya pamoja