Kambibi Kamugisha kutoka CDF akisisitiza jambo katika maadhimisho ya siku ya wanawake ambapo shirika hili limeadhimisha maadhimisho hayo katika kata ya Nyanungu kupitia Michezo ambayo ilikuwa ni siku ya Michezo kwa kwao kwa kushirikiana na shirika la RIGHTOPLAY ambapo amezidi kusisitiza jamii kuondokana na mila zinazokandamiza mtoto wa kike.
Kauli mbiu ya Mwaka huu inasema Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi hivyo kupitia kauli mbiu hiyo mtoto wa kike hana budi kutimiza ndoto yake ya kimasomo ili kuendana na kaulimbiu , ameiomba jamii kuondokana na tabia za kuodhesha mabinti katika umri mdogo.
|