MFUMUKO WA BEI WA MWEZI JANUARI 2017 WAONGEZEKA.
Mkurugenzi wa Sensa
na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim
Kwesigabo, akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017
unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8
ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba
2016.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi
wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati
akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.
Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei
kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na
bidhaa zisizo za vyakula.
Alitaja baadhi za vyakula
zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia
6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi
vitamu kwa asilimia 6.5.
Alisema kwa upande mwingine baadhi ya
bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni
pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.
Kwesigabo alisema thamani ya shilingi
ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania
ingeweza kununua katikavipindi tofauti.
"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa
zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma hupungua" alisema Kwesigabo.
Alisema uwezo wa shilingi 100 ya
Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti
42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20
ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)