KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA MAMIA KUMZIKA MNEC WILAYANI SAME.
Kaimu katibu
UVCCM Shaka Hamdu Shaka akimpokea Katibu mkuu wa CCM Abdrahman Kinana
alipowasili katika mazishi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa
Marehemu Ally Mbaga wilayani Mwanga alieyefariki kwa ajali ya gari
wakati anatoka katika maadhimisho ya Miaka 40 ya CCM wilayani Rombo,
Kilimanjaro.
Katibu Mkuu CCM
Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu Nyeupe,katibu wa CCM Mkoa wa
Kirimanjaro wa kwanza kushoto pamoja na Kaimu katibu Uvccm Shaka hamdu
shaka wakielekea Eneo la Msiba pamoja na makada mbali mbali wa Chama
cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu akisalimiana na Kiongozi wa Familiya ya Marehemu Ally Mmbaga.
Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana aliye valia vazi la kanzu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadick.
"Kwa niaba ya
Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk John Pombe Magufuli na Chama Cha
Mapinduzi nawasilisha kwenu salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na
wanafamilia yote ya Ndg Mmbaga kufuatia msiba huu mzito ambao
umewagusa kuwapa huzuni na majonzi makubwa yasiolelezeka kwa kupoteza
nguzo muhimu tuliokuwa tukishirikiana katika mambo mbali
mbali"Alisema Katibu Mkuu wakati akiwasilisha salamu za rambi rambi za
Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki
kuswalia jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Mwalimu Ali
Mbaga wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha
Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo. Mbaga ni
miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati
wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.
Katibu Mkuu wa
CCM Abdulrahman Kinana Aliye vaa Vazi la kanzu Katikati pamoja na
Viongozi wananchi wakitoka Kuuzika Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC,
Mwalimu Ali
Mbaga aliyezikwa leo katika kijiji cha
Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro
PICHA NA FAHADY SIRAJI UVCCM