HILI NDILO JIJI LA MWANZA WAKATI WA MVUA

Pichani ni moja ya barabara za Jijini Mwanza baada ya mvua kunyesha jana. Ilikuwa ni kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo inayotoka Soko Kuu

Uzoefu unaonesha kwamba mitaro kujaa uchafu husababisha kero hiyo wakati wa mvua.
Bado kuna lawama kwa baadhi ya wanaofanya biashara katika maduka yaliyo kwenye barabara za Jijini Mwanza kwamba wamekuwa wakitupa uchafu katika barabara hizo na kusababisha kuziba mara kwa mara huku lawama nyingine zikiwaendea baadhi ya wanaofanya usafi kwa kufagia uchafu kuelekea kwenye mitaro hiyo

Halmashauri ya Jiji la Mwanza inapaswa kuliona hili kama tatizo na kuja na mbinu mbadala ikiwemo faini kali kwa atakayekutwa akitupa ovyo uchafu.
 
#BMGHabari

Powered by Blogger.