WENJE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA KANDA YA ZIWA.
Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Ezekiel Dibogo Wenje
(Chadema 2010/15) amechaguliwa kwenye mkutano mkuu wa Kanda ya Ziwa
Victoria, kuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda hiyo.
Wenje
alimshinda Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Chief
Kalumuna ambapo Uchaguzi huo ulifanyika jana Januari 18,2017 Jijini
Mwanza na matokeo kutangazwa majira ya tatu usiku.
Katika uchaguzi
huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilichukuliwa na Ansbert Ngurumo ambapo
viongozi mbalimbali wa Chadema Taifa akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe,
walihudhuria mkutano.
Binagi Media Group
Binagi Media Group