(PICHA
NA IDARA YA HABARI/WHUSM)
Na
Shamimu Nyaki-WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano
Barani Afrika katika kuhabarisha umma.
Waziri
Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara
katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.
“Fanyeni
kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa
watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa
mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya
Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na
watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza
mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi
kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.
Aidha,
Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya
Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea
kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.
“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani
zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa
tukirusha matukio mubashara kupitia
mitandao ambayo
yana wafuatiliaji zaidi ya million
tano.” Alisema Dkt.Ryoba.
Shirika
hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje
ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.