Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza mmoja wa wataalam
walioambatana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad (wa
tatun kulia) walipomtembelea ofisini kwake leo ( 10/01/2017) jijini Dar Es
Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. sifuni Mchome (wa kwanza kushoto)
akifafanua jambo wakati wa kikao na Balozi wa Norway na ujumbe wake (hawapo
pichani) walipotembelea Wizara hiyo leo ili kujadili namna wataalam hao
wanavyoweza kusaidia kiteknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa haki kwa
wananchi.
Waziri wa
Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Balozi
wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad na ujumbe wake baada ya kumaliza
kikao leo jijini Dar es salaam.