Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alfred Maruma wa jimbo
Katoliki la Njombe, wakati alipotembelea shamba ya chai ya wakulima wa
kijiji cha Lwangu, Njombe
Picha/habari na OWM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali imejipanga katika kuhakikisha inaongeza thamani ya mazao yake
kabla ya kuyauza nje ya nchi.
Amesema kwa muda mrefu Serikali ilikuwa inapata hasara kwa
kusafirisha malighafi nje nchi lakini kwa sasa inajenga viwanda ili iweze kuuza
bidhaa.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 25,
2017) wakati alikizungumza na wakulima wa chai katika kijiji cha Lwangu
wilayani Njombe.
“Miaka mingi Serikali imekuwa ikipata hasara kwa kuuza mazao nje
ya nchi, tumeamua kujenga viwanda vitakavyoweza kuyachakata na kuuza bidhaa
badala ya malighafi,”.
“Ujenzi wa viwanda ni moja kati ya mikakati dhati ya Serikali ya
kuhakikisha mazao mnayolima yanakuwa na thamani
kubwa hivyo kuwaongezea tija,”
alisema.
Kutokana na mkakati huo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuongeza
juhudi katika kilimo. “Kuna anayetaka hela hapa? Kama mnataka mali mtazipata shambani.
Limeni,”.
Waziri Mkuu alisema mazao hayo ndiyo yatakayoweza kuleta tija kwa
wakulima, hivyo aliwashauri waendelee kushirikiana katika vikundi ili wapate
misaada ya kitaalam kwa urahisi.
Aidha, alimuagiza mkuu wa wilaya hiyo, Ruth Msafiri na Maafisa
kilimo kuwatembelea wakulima hao kwa lengo la kuwaelekeza namna bora ya
kuendeleza mazao yao.
Waziri Mkuu alisema hatua hiyo itawawezesha wakulima kupata mbinu
bora za kilimo na hatimaye kuvuna mazao mengi yenye viwango vya ubora
vinavyotakiwa kimataifa.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliiagiza halmashauri
ya wilaya ya Njombe kuwaunga mkono wakulima hao kwa kuimarisha barabara
zinazoingia kwenye mashamba yao.
“Tuwaunge wakulima wetu kwa kuwaimarishia miundombinu ya barabara
ili kuwawezesha kupeleka chai yao kiwandani kwa gharama nafuu,” alisema.
Naye Mbunge wa jimbo la Lupembe Mheshimiwa Joram Hongoli alisema
kilimo cha chai ndio mkombozi kwa wananchi hao, hivyo aliwaomba waongeze juhudi.
Awali Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kutoa Huduma kwa Wakulima Wadogo
Njombe (NOSC), Bw. Filber Kavia alisema kampuni inatoa huduma za kitaalam kwa
wakulima.
Alisema wanalenga kuendeleza kilimo cha chai kwa kuongeza kuongeza
uzalishaji kwa hao kutoka kilo 500 hadi kilo 2,000 za majani makavu ya chai kwa
hekta kwa mwaka.
Meneja huyo alisema kampuni inakusudia kuongeza mashamba mapya ya
chai hadi kufikia hekta 3,800 kutoka hekta 614 ifikapo mwaka 2025.
Bw, Kavia alisema huduma nyingine inayotolewa na kampuni hiyo ni
utoaji wa mikopo nafuu ya pembejeo bila ya riba na mkulima hulipa muda mrefu
kupitia mauzo ya chai.
Pia kampuni hiyo inatoa huduma ya usimamizi wa mashamba makubwa ya
chai ya vijiji na watu binafsi kwa mkataba maalumu ili kuongeza uzalishaji na
tija.
Awali Waziri Mkuu alikagua eneo litakalojengwa kiwanda cha kisasa
cha kuchakata chai cha kampuni ya Unileve
|