UONGOZI MPYA WA CHAMA CHA SOKA MKOANI ARUSHA WAPANIA KUNYANYUA SOKA MKOANI HUMO.
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Arusha (ARFA) Peter Temu.
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha soka
Mkoa wa Arusha (ARFA) kimefanikiwa kupata uongozi mpya baada ya uchaguzi
mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki wilayani Monduli
ambao watakaa madarakani kwa miaka minne ijayo.
Katika uchaguzi
huo uliokuwa unawaniwa nafasi kumi, ulionekana mgumu kwa nafasi mbili
pekee ile ya Mwenyekiti pamoja na nafasi ya Mjumbe wa mkutano mkuu wa
TFFambapo wagombea walikua wawili wawili.
Waliofanikiwa
kupita katika uchaguzi huo kwa nafasi ya mwenyekiti ni Peter Temu
aliyemshinda Omary Walii kwa kura 13 kwa 6, Katibu mkuu Zakayo Mjema
aliyepata kura 18, katibu msaidizi akipita Nassoro Mwarizo.
Nafasi ya Mweka
hazina ikienda kwa Omary Nyambuka, Huku nafasi ya Mjumbe wa mkutano
mkuu wa TFF Issa Hamisi alimshinda Athumani Mhando kwa kura 13 kwa 8, na
nafasi ya kamati tendaji ya ARFA ikienda kwa Soud Abdy.
Washiriki ambao
ni wajumbe wa vyama vya soka kutoka Mkoani hapa waliojitokeza ni kutoka
Arusha Mjini, Monduli, Arumeru, Karatu, Longido, FRAT ambao walifanya
jumla ya wajumbe 19 waliopiga kura.
Huku nafasi ya
wajumbe watatu wa kamati tendaji iliyopata mtu mmoja na mwakilishi wa
vilabu ambazo hazajajazwa utafayika uchaguzi mdogo baada ya siku 90
kupita alisema katibu wa kamati ya Uchaguzi Seleimani Kirua
Katibu mkuu
mpya wa ARFA Zakayo mjema. alisema wameingia madarani huku kukiwa na
deni kubwa la kuitendea haki Arusha ili kuweza kurudisha timu ligi
kuu.
"Kwanza
nashukuru nimechuguliwa kwa idadi kubwaya kura na hii ni dhahiri wajumbe
wameniamini na nitahikisha tunashirikiana kwa pamoja na wilaya zetu
katika kuhakikisha soka la mkoa huu linarejea kama ilivyokuwa
zamani,"alisema Mjema.
Mwenyekiti mpya
Peter Temu aliwasihi wadau wa soka wawe na matumaini kuwa mpira
utarejea kulingana na safu mpya yenye morali ya wa kusaidia na
kuendeleza mpira.