UJIO WA NYANZA FESTIVAL 2017 JIJINI MWANZA WAPAMBA MOTO.
Kikao cha maandalizi cha Tamasha kubwa
la Nyanza Festival kikifanyika Jijini Mwanza, kikiongozwa. Ni tamasha
litakalowahusisha wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya.
Picha na Nyanza Festival 2017
Mkurugenzi wa kampuni ya Famara
Entertainment, Fabian Fanuel (mwenye kofia) na wajumbe wengine wakiwa
kwenye kikao cha maandalizi ya tamasha la Nyanza Festival 2017
Wanakamati wa Nyanza Festival wakipitia miswada mbalimbali ili kufanikisha tamasha hilo mapema mwaka huu
Wanakamati wa Tamasha kubwa la Nyanza Festival 2017
Na Binagi Media Group
Nyanza Festival 2017 ni tamasha kubwa
la muziki wa kizazi kipya linatorajariwa kufanyika kwa mara ya kwanza
Jijini Mwanza na baadaye kusambaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa,
Tanzania na nje ya Tanzania.
Ni wazo ambalo lilitoka kwa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Famara Entertainment ya Jijini Mwanza, Fabian
Fanuel na kupokelewa vyema na wadau wote wa muziki mkoani Mwanza
wakiwemo watangazaji, waandishi wa habari, wanamuziki, Madjz, wamiliki
wa mitandao ya kijamii (blogs), watayarishaji wa muziki na wengine
wengi.
"Tamasha hili litaongeza chachu ya
kuikuza sanaa ya muziki ikizingatiwa kwamba upele umepata mkunaji maana
linaandaliwa na wahusika wenyewe ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika
kukosa fursa ya kutumbuiza kwenye matamasha ambayo yamekuwa
yakifanyika". Fanuel ameiambia BMG.
Itakumbukwa kwamba kampuni ya Famara
Entertainment kwa miaka miwili mfululizo tangu mwaka juzi, imejijengea
heshima kubwa kwa kufanikisha tamasha la dini liitwalo "La Kwetu
Concert" katika uwanja wa CCM Kirumba na sehemu ya mapato yake kusaidia
wahitaji katika jamii wakiwemo watoto wenye ualibino.