TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA DCP: AHMED MSANGI ANATOA
TAHADHARI KWA WANANCHI WOTE WA MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIHADHARI/KUJIEPUSHA
NA WATU/VIKUNDI VYA WATU AMBAO NI WAHALIFU WALIOKUSUDIA KUJIPATIA FEDHA NYINGI
TOKA KWA WANANCHI KWA KUWADANGANYA/ KUWARUBUNI WAJIUNGE NA BIASHARA YA UPATU
AMBAPO WANANCHI HAO HUSHAWISHIWA KUWEKEZA FEDHA KIDOGO KWA MUDA MFUPI KATIKA
VIKUNDI HIVYO NA BAADA YA HAPO WANAAHIDIWA KULIPWA FEDHA NYINGI ZAIDI YA ZILE
WALIZO WEKEZA BILA KUFANYA KAZI YEYOTE. BIASHARA HIYO INATAMBULIKA KWA JINA
LISILO RASMI LA KUPANDA MBEGU NA KUVUNA.
HIVI KARIBUNI KUMEJITOKEZA WIMBI KUBWA LA VIKUNDI VYA NAMNA
HIYO HAPA JIJI MWANZA NA TAYARI WANANCHI WENGI WAMEIBIWA FEDHA ZAO. KUTOKANA NA
KUONGEZEKA KWA UHALIFU WA AINA HII JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LIMEANZISHA
NA LINAENDELEA NA MISAKO MAENEO MBALIBALI YA JIJI NA MKOA WA MWANZA, KWA LENGO
LA KUBAINI NA KUWAKAMATA WATU/VIKUNDI VINAVYOFANYA UHALIFU HUO. (UPATU)
AIDHA KAMANDA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU VIKUNDI
VIFUATAVYO AMBAVYO UPELELEZI UMEONESHA KUWA VINAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU
AMBAVYO NI; KIKUNDI KINACHOJULIKANA KWA JINA LA AQ POWER CLUB
KINACHOMILIKIWA NA HAPPY ALOYCE MBUYA
MIAKA 35, MCHAGA , MKAZI MTAA WA ILIEMELA ENEO LA MAHAKAMANI, MFANYABIASHARA NA
MKURUGENZI WA KAMPUNI BINAFSI IITWAYO AQ CUMPUTER CO.LTD, UPELELEZI UMEBAINI
KWAMBA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKISHIRIKIANA NA WENZAKE SABA (7) WAMEFANIKIWA
KUKUSANYA FEDHA ZAIDI YA TSH 100,000,000/= KUTOKA KWA WANANCHI AMBAO
WALISHAWISHIWA KUJIUNGA NA KIKUNDI CHAKE, PIA UPELELEZI UMEBAINI KUWA AQ POWER
CLUB SIO TAASISI ILIYOSAJILIWA KISHERIA BALI JINA LA BIASHARA LA MTUHUMIWA.
TAYARI MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU NA WENZAKE SABA WAMEKAMATWA
NA UPELELEZI UNAENDELEA PINDI UKIKAMILIKA JARADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA
SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA DHIDI YAO, AIDHA KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MWANZA ANATAHADHARISHA WANANCHI KUHUSU SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA KIKUNDI/ KAMPUNI
BINAFSI YA BEGA KWA BEGA MICRO FINANCE COMPANY LTD, KWANI WATU WENGI WAMEKUJA
KURIPOTI POLISI JUU YA KUTAPELIWA FEDHA ZAO NA KAMPUNI HIYO, TAYARI JESHI LA
POLISI MKOA WA MWANZA LIMEWATIA MBARONI WAKURUGENZI NA BAADHI YA WAFANYAKAZI WA
KAMPUNI HIYO NA MAJALADA YA KESI HIZO YAPO KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA
HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
AIDHA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUZIFANYIA KAZI TAARIFA ZA
KIINTELEJENSIA KUHUSU TAASISI ITAMBULIKAYO KWA JINA LA AMKA MWANAMKE (AMWA),
KWAMBA PIA INAJIHUSISHA NA BIASHARA YA UPATU, UCHUNGUZI UNAFANYWA ILI KUWEZA
KUBAINI UKWELI WA TAARIFA HIZO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANAWATAHADHARISHA WANANCHI WOTE WA
MWANZA NA MAENEO JIRANI KUJIEPUSHA NA VIKUNDI VYA AINA HII, PIA ANAWAAASA
WANANCHI KUJITAFUTIA KIPATO CHA HALALI KWA KUFANYA KAZI HALALI NA SIO KUWEKEZA
FEDHA KIDOGO (KUPANDA) NA KUTARAJIA KUPATA FEDHA NYINGI KWA MUDA MFUPI (
MAVUNO). TAMAA YA KUPATA UTAJIRI WA HARAKAHARAKA UMEWAINGIZA WANANCHI WENGI
KWENYE HASARA KUBWA ILIYO TOKANA NA KUIBIWA FEDHA ZAO KWANI HAKUNA KIKUNDI/ MTU
ANAYEWEZA KUPEWA FEDHA KWA MUDA MFUPI ALAFU BAADA YA MUDA MFUPI ALIPE FEDHA
NYINGI ZAIDI. WANANCHI WATAMBUE KUWA HUU NI MTEGO WA WAHALIFU WA KUWAFANYA
WANANCHI WASHAWISHIKE KUJIUNGA NA VIKUNDI HIVYO ILI WAWAIBIE.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA