NOMA SANA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2017 ZANZIBAR.
Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara
Bw.Yusuf Mahmoud akionesho moja ya kitabu chenye mambo lukuki yahuso
tamasha hilo pamoja la habari mbalimbali za wasanii watakaotumbuiza
kwenye tamasha hilo la aina yake kwa wakazi wa Zanzibar na wageni
waalikwa kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje.
Na Joachim Mushi
Mwanamuziki mkongwe mwenye makazi yake
ya kimuziki nchini Japan Fresh Jumbe akizungumza na waandishi wa habari
mapema kuhusu ushirika wake pamoja na bendi yake nzima katika tamasha la
sauti za busara.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za
Busara Bw. Simai M. Said wa pili kutoka kushoto akiwa anaongea na
waandishi wa habari juu ya Tamasha la 14 la sauti za busara.
Mkurugenzi wa Tamasha la 14 la Sauti za
Busara, Bw. Yusuf Mahmoud (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es salaam huku akitaja baadhi ya wanamuziki ambao
watatumbuiza 'Live' katika Tamasha hilo.
Jumla ya wasanii 400 wa Ki-Afrika toka takribani makundi 40 wanatarajia kutumbuiza katika Tamasha la Sauti za Busara 2017. Tamasha hilo litakaloanza kufanyika tarehe 9-12 ya mwezi Februari 2017 litafanyika Mji Mkongwe, Zanzibar.
Akizungumza Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Bw. Yusuf Mahmoud alisema Tamasha litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morrocco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha.
Muziki unalateta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali. Duniani na ujumbe mkubwa kwa Dunia ni kuwa muziki unakuza umoja na urafiki hata kwenye mipaka ya sehemu mbalimbali. Alisema Tamasha la 14 la Sauti za Busara kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha hilo, lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ mwaka huu tamasha litakua na majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa/nyumbani.
Watu mbali mbali wenye rangi tofauti, umri tofauti kwa mara nyingine tena wataunganishwa na tamasha kusheherekea muziki wa ki-Afrika. Matarajio ya mahudhurio ni makubwa kutoka Tanzania na nje ya Nchi kufatia kujaa kwa sehemu za malazi Mji Mkongwe kwa wiki ya tamasha. Wasanii wote watatumbuiza ‘live’ muziki wa Ki-Afrika kila siku kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 7:00 usiku.
Lengo la tamasha ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanzania ni Sh 6,000 kwa siku na Sh20,000 kwa siku nne za tamasha. Tamasha hili ambalo kwa asilimia 100 huwa live kitu ambacho kinalifanya tamasha hili liwe la kipekee huwapakipaumbele wanamuziki chipukizi kutambulisha kazi zao zenye kutambulisha uhalisia wa utamaduni.
Tamasha la Sauti za Busara hukutanisha wataalamu wa muziki wa kimataifa na kutoa nafasi kw amuziki wa Afrika Mashariki kufwakifikia watu mbalimbali dunia nzima kupitia jukwaa la Sauti za wanamuziki wa nyumbani amabao hutumbuiza tamashani hupata mialiko kushiriki matamasha mbali mbali Barani Ulaya na Afrika.
"...Ndani ya siku hizo nne jumla ya wasanii 400 wa ki-Afrika (makundi 40) yatatumbuiza tamasha Sauti za Busara 2017. Tamasha litaanza na gwaride kutoka maeneo ya Kisonge (karibu na Michenzani) kuanzia saa 9:00 jioni Alhamis tarehe 9/2. Tamasha litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morrocco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha. Muziki unalateta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali. Duniani na ujumbe mkubwa kwa Dunia ni kuwa muziki unakuza umoja na urafiki hata kwenye mipaka ya sehemu mbalimbali," alisema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Bw.Yusuf Mahmoud.
Kati ya makundi 40 nusu yanatoka Tanzania. Makundi hayo ni Afrijam Band, CAC Fusion, Chibite Zawose Family, Cocodo African Music Band, Jagwa Music, Matona's G Clef Band, Mswanu Gogo Vibes, Rajab Suleiman & Kithara, Tausi Women's Taarab, Usambara Sanaa Group, Wahapahapa Band, Ze Spirits Band.
Tuna hakika makundi kama haya yatawakilisha vema matamasha ya nje endapo yatapata nafasi, Makundi mengine ni pamoja na Batimbo Percussion Magique (Burundi), Bob Maghrib (Morocco), Buganda Music Ensemble (Uganda), Grace Barbe (Seychelles), H_art the Band (Kenya), Imena Cultural Troupe (Rwanda), Isau Meneses (Mozambique), Karyna Gomes (Guine Bissau), Kyekyeku (Ghana), Loryzine (Reunion), Madalitso Band (Malawi), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Rocky Dawuni (Ghana), Roland Tchakounté (Cameroon), Sahra Halgan Trio (Somaliland), Sami Dan and Zewd Band (Ethiopia), Sarabi (Kenya), Simba & Milton Gulli (Mozambique).
Shukrani zetu za dhati na za kipekee tunazifikisha kwa Hotel ya Golden Tulip kwa kuhakikisha kikao hiki kinafanikiwa. Pia tunawashukuru ninyi wote mliohundhuria kikao hiki na kuhakikisha mnafikisha taarifa zetu kwa wananchi. Wadhamini wa tamasha hili ni pamoja na Africalia, Chuchu FM Radio, Zanlink and Coastal Aviation Embassy of Germany, Ethiopian Airlines, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Memories of Zanzibar, Mozeti, Music In Africa, Norwegian Embassy, Pro Helvetia, Swiss Agency for Development & Cooperation (SDC), Tifu TV, na wengine wengi.