Simu ya mkononi nusura imtoe roho mke wa mtu Rorya
Mkazi wa Nyang’ombe kata ya Nyamagaro wilayani Rorya mkoani Mara Joyce Akote (29) amenusurika kifo
baada ya kunywa sumu kutokana na kukutwa na mume wake akiongea na simu ambayo
mumewe aliitilia mashaka kuwa ya usaliti.
Akote alichukua maamuzi hayo magumu januari 21 baada ya mume
wake kumtaka aeleze alikuwa akiongea na nani jambo ambalo alikataa kulitekeleza
hivyo kuamua kutaka kujiondoa uhai.
Ndevi Maziku ambaye ni mume wake alisema kuwa mke
wake aliamua kunywa sumu baada ya kuulizwa kuhusiana na simu ya mkononi,
na makosa aliyokuwa anayafanya wakati akipigiwa alikuwa akitaka
kuipokea alikimbia kujificha.
Maziku alisema kuwa hali hiyo ilikuwa inampa utata na
ndipo alipoanza kuhoji kulikoni lakini kikawa ni chanzo cha yeye kumtishia kuwa
asimfuatilie .
“Ukiendelea kuniuliza uliza nitakuonyesha kitendo ambacho
hutakisahau maishani mwako, nikataka kujua kwa nini afanye vile lakini
nikahisi kuwa alikuwa na mahusiano na mume mwingine nje,” alisema Maziku.
Hata hivyo baada ya kubainika kuwa amekunywa sumu
alikimbizwa zahanati kunusuru maisha yake na kuokolewa ndugu zake
mwanamke walimfata ambapo mme wake hakutaka tena kurudiana na mke wake na hapa
joto la asubuhi limezungumza na mwanaume huyo.
“Alisaga betrii akanywa, lakini namshukuru Mungu tulimkimbiza
katka zahanati ya Nyamagaro tukaokoa maisha yake, na sasa amekimbia kwenda
Kenya baada tu ya kupata fahamu,”alisema Maziku.
Hata hivyo Maziku alisema maisha yake na mke na wake tangu
amuoe mwaka 2015 siyo mazuri kwani amekuwa hamsikilizi kama mume alikuwa
akijiamulia nini afanye kwa wakati wake ambapo wakati mwingine alikuwa
akiondoka bila hata kuaga.
Shuhuda wa tukio hilo James Makanga alisema baada ya
Akote kubainika kuwa amekunywa sumu alishiriki kumkimbiza zahanati ambapo
alipata huduma ya kitabibu na kurejea katika hali yake ya uzima.
“Maziku ni jirani yangu, walikorofishana na mke wake ambaye
alikunywa sumu tukamkimbiza zahanati ambapo alinyweshwa mziwa na kumwekea tripu
ya maji, alipata fahamu akatoroka kurudi nyumbani na ndugu zake kutoka Kenya
wakaja kumchukua,”alisema Makanga.
Mwenyekiti wa kijji cha Muharango Jumanne
Nyabori alisema kuwa alipopata taarifa ya tukio hilo alitoa maelekezo ya kwenda
kituo cha polisi lakini hawakufanya hivyo.
“Matukio kama haya siyo mengi lakini wananchi wanapaswa kuwa
makini na kuacha kuchukua maamuzi magumu kama haya ya kutaka kuondoa maisha
yao, tunamsubiri arudi kutoka kwao ili sheria ifuate mkondo wake,” alisema
Nyabori
Wakati huo huku katika kijiji hicho
aliyefaamika kwa jina la Pius Kuhuri mwenye umri wa miaka 17
mkazi wa kijiji cha Muhalango kata ya Nyamagalo Wilayani Rorya Mkoani Mara amekutwa
ameafrika dunia kwa kujinyonga na kamba ya katani ndani ya Nyumba
Chanzo cha tukio hilo hakijafaamika
na tukio hilo ni la pili ndani ya Mwezi mmoja amesema diwani wa kata hiyo Ezra
Masana.