Serikali yaunda Tume kubaini chanzo cha Moto JNIA

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto  usiku wa kuamkia leo( jana) katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ,kulia ni Mkurugenzi wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha.

Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo .

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua chumba cha kuhifadhia abiria kilichoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo ,wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire.(Picha na Benjamin Sawe)

Na: Benjamin Sawe
Serikali  imeunda Tume ya uchunguzi ya watu 12 ili kuweza kuchunguza na kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyotokea jana saa Tano usiku katika chumba kidogo cha kuhifadhia mizigo kilichopo kwenye jengo la Pili la abiria (Terminal II) katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa  Tume hiyo iliyoundwa inaongozwa  na Joseph Nyahende ambae anatoka katika ofisi za  Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.
“Ninategemea kupata ripoti ya kitaalamu kutoka kwa Tume hii, ili kutusaidia kubaini kiundani juu ya chanzo haswa kilichopelekea moto huu”, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa huduma katika jengo hilo  zinaendelea kama kawaida ambapo awali zilisitishwa na kuhamishiwa katika Jengo la Kwanza la abiria (Terminal I).
“Mara baada ya moto kutokea, kitu cha kwanza kilichofanyika ni kuudhibiti moto huu ili usiweze kusambaa katika maeneo ambayo hayajaathirika, kisha tukatafuta njia za kurudisha huduma kwa abairia”, amesisitiza Profesa Mbarawa.
Powered by Blogger.