NAIBU WAZIRI WA MICHEZO AHUDHURIA MCHEZO WA KUMUENZI MCHEZAJI WA MBAO FC ALIYEFARIKI UWANJANI.
Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, jana
akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Mhe.Nape Nnauye, kwenye
mchezo wa hisani kati ya timu za UMISETA wilaya za Nyamagana na Ilemela
mkoani Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Mhe.Wambura,
alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA na
kwamba imejipanga vyema ili kuiendeleza michezo hiyo mwaka huu 2017 kwa
kuondoa dosari zote zilizojitokeza hapo awali na kusababisha kuahirishwa
mwaka jana.
Lengo la mchezo
huo ilikuwa ni kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya vijana
chini ya miaka 20 ya Mbao Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, Isamail Khalifan Mrisho ambaye Disemba 04 mwaka jana, alifariki
dunia akiwa uwanjani kwenye mchezo baina ya na timu yake na Kagera Sugar
huku kiingilio kilichopatikana kwenye mchezo huo kikiwasilishwa kwa
familia ya mchezaji huyo.
Mchezo huo
uliandaliwa na taasisi ya soka nchini iliyomlea mchezaji huyo ya The
Football House kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya Mbunge wa Jimbo
la Ilemela, Mama Angelina Mabula iitwayo Angeline Foundation.
Hadi dakika 90
zinatamatika, timu ya kombaini ya Nyamagana iliibuka mshindi kwa ushindi
wa mabo2-1. Mabao ya Nyamagana yalifungwa na Rajesh Kotecha na Kuzaifa
Mdabiru huku Ilemela wakipata bao la kufutia machozi baada ya mchezaji
wa Nyamagana Jefta John kujifunga.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, alisema Serikali haijayafuta
mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA hivyo imejipanga vyema mwaka huu
ili kuendeleza michezo hiyo mwaka huu kwa kuondoa dosari zilizojitokeza
hapo awali na kusababisha mwaka jana kuahirishwa.
Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald
Masele, alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inaendeleza mchezo wa
soka ambapo imeanzisha timu kwa kila soko la machinga wilayani humo
hatua ambayo itasaidia kuukuza mchezo huo.
Mkurugenzi wa taasisi ya The Football
House, Mbaki Mutahaba, alisema taasisi hiyo itaendelea kumuenzi mchezaji
wake Ismail Khalifan Mrisho huku akiwasisitiza vijana kutumia vyema
vipaji walivyonavyo kama ilivyokuwa kwa Mrisho ambaye ameacha alama ya
soka nyuma yake baada ya umauti kumkuta.
Kaka wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho,
aitwaye Athman Kitwana, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya familia
kwa namna ambavyo wadau mbalimbali walivyojitoa kumwendeleza kipaji
chake, kusaidia kwenye msiba wake na namna wanavyoendelea kumuenzi baada
ya umauti.
Wazazi wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, kushoto ni Rehema Mfaume (mama) na kulia ni Khalifan Mrisho (baba)
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, pamoja na viongozi wengine
wakimkumbuka marehemu Ismail Khalifan Mrisho.
Wanaamilia wakimkumbuka marehemu Ismail Khalifan Mrisho.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akisalimiana na wasimamizi wa mchezo huo
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akisalimiana na wachezaji wa Kombaini Nyamagana
Viongozi wa taasisi ya The Football House wakisalimiana na wachezaji
Kombaini UMISETA Ilemela (jezi nyeupe), wakisalimiana na Kombaini UMISETA Nyamagana
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akipiga mpira kuashiria ufunguzi
wa mchezo baina ya Kombaini Nyamagana na Ilemela
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akipiga mpira kuashiria ufunguzi
wa mchezo baina ya Kombaini Nyamagana na Ilemela
Mpambano baina ya Kombaini Ilemela na Nyamagana ultamatika kwa Nyamagana kuibuka na ushindi wa bao 2-1
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari Nyamagana na Ilemela wakifuatilia mchezo baina ya Kombaini Ilemela na Nyamagana
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, akizungumza kabla ya mchezo huo.
Afisa Michezo Jijini Mwanza, Mohamed Bitegeko, akizungumzia mchezo huo
Afisa Michezo Manispaa ya Ilemela, Bahati Sosho Kizito, akizungumzia mchezo huo
Baadhi ya viongozi wa taasisi ya The
Football House, wakiwa na wadu wengine kwenye mchezo huo baina ya
Kombaini Ilemela na Nyamagana uliomalizika kwa Nyamagana kuibuka na bao
2-1 kwenye dimba la CCM Kirumba.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG