SERIKALI YAMALIZANA NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA....SASA RUKSA KUTUMIA MIHURI
Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa
Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia
mihuri kwa wenyekiti wa serikali za mitaa.
Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali
za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene
amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa
Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.
''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu
Wenyeviti, lakini kama mihuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona
kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili"
amesema
Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu
za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na
matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na
kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.
Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha
ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi.