SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI NCHINI KATIKA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye
vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea
utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
|
Picha/ Habari na Raymond Mushumbusi
Serikali
imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari
kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika
kutekeleza majukumu yake.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa Kampuni
ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv pamoja na
Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina ya
Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa
wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika
kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.
“Niseme
kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu kutoka
kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa Serikali
imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika kuhabarisha umma wa
watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.
Kawa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali
Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika
kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo vyote vya Mawasiliano
Serikalini.
Dkt
Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya Mawasiliano
serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu Serikali.
“Niwahakikishieni
ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka Serikali
litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya
Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu” alisisitiza
Dkt Abass.
Aidha
Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bibi. Joyce Mhavile ameishukuru Serikali kwa kuendelea
kushirikiana na Vyombo vya Habari vya binafsi nchini katika kutoa taarifa kwa
umma ambazo zimesaidia kuelimisha, kuburudisha na kutengenza mazingira ya watu
kuamini yale yanayotolewa na vyombo vyao.
Naye
Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba ameipongeza
serikali kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari nchini na kuahidi kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali
katika upashanaji habari.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika ziara
ya siku sita kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji kazi wa vituo
hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna bora ya kuiendeleza
sekta ya habari kwa manufaa ya taifa.