SEIKALI KUWACHUKULIA HATUA WANAOSHINDWA KUPAMBANA NA UVUVI HARAMU.
Habari/Picha na
Beatrice Lyimo
Serikali
imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia
hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi
haramu.
Akizungumza
baada ya kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba za Maliasili, Ulinzi,
Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya Ndani
Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia agenda ya
kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao.
Alisema
kuwa maafisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia
ni kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia
mabomu.
“Kuna
baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia
kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa
katika nyazifa hiyo”.
Kwa
upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema
kuwa nchi yetu inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na
changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka
katika kupambana na uharamia huo.
Akifafanua
zaidi kuhusu hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa
jambo la uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi wa
nchi hivyo lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa.
Alisema
ni aibu kwa taifa letu la Tanzania kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi
nyingi kwa sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.
Naye
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania
wote kushirikiana na Serikali katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi
haramu.
Mwigulu
Nchemba alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika
kulinda rasilimali za majini tulizo nazo”.
Kikao
hicho ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu ambapo
maazimio hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita kwa
ajili ya kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale
patakapoonekana pana changamoto.