LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU WALIOMTABIRIA KIFO
Waziri
Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa, amesema kuwa Serikali ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), ina watu wenye roho mbaya kwani waliwahi kumuombea
kifo,lakini hadi leo anadunda.
Lowassa ambaye alikuwa mgombea urais wa Chadema na kuungwa mkono na
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa), amesema baadhi ya
waliomwombea kifo leo hawapo duniani,kwani mungu ndiye anayepanga maisha
ya mwanadamu.
“Kule kwa wenzetu kuna watu wenye roho mbaya,kwani hata mimi waliniombea
kifo,waliniombea kifo muda mrefu kweli lakini mpaka sasa bado nadunda
tu wakati baadhi ya walioniombea hivyo,leo hawapo duniani kwa mapenzi ya
mungu”alisema Lowassa.
Lowassa aliyasema hayo jana baada ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano
wa ufunguzi wa uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Matevezi jimbo la
Arumeru Magharibi,kupaza sauti wakimuuliza juu ya hatima ya mbunge wao
Lema ambaye yupo Gereza la kisongo kwa miezi miwili sasa.
Katika hatua nyingine, Lowassa aliwataka timu ya kampeni na wananchi
kuhakikisha kura haziibiwi kwa kile alichoeleza kuwa Chadema ina nguvu.