RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI


Rais wa  Uturuki,  Mheshimiwa  , Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 22, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifurahia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli.
Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan akiagana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kumfikisha kwenye hoteli ya Serena  jijini Dar es salaam  baada ya kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam na kumsindikiza hadi kwenye hoteli hiyo alikofikia Januari 22, 2017. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Powered by Blogger.