MVUA ZILIZOAMBATANA NA UPEPO ZABOMOA DARASA NA NYUMBA YA MWALIMU SHULE YA MSINGI NYAMWIGULA

DIWANI WA KATA YA BINAGI MARWA MALIGILI AKIONESHA DARASA AMBALO LIMEBOMOLEWA NA MVUA ZILIZOAMBATANA NA UPEPO MKALI JANA KATIKA SHULE YA MSINGI NYAMWIGULA.

Kutokana na Mvua ambazo zimeanza kunyesha na kuambatana na upepo mkali Nyumba Moja ya Mwalimu wa shule ya Msingi Tumaini na Darasa moja katika Shule ya Msingi Nyamwigula Wilayani Tarime Mkoa Mara  vimebolewa ikiwa tukio hilo ni la pili kuikumba shule hiyo ambapo mwaka jana mvua ambayo iliambatana na upepe mkali  iliezua vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ya Walimu.

Baada ya tukio la mwaka jana kuezuliwa ofisi ya walimu jambo hilo limechangai walimu wote akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamwigula  kutumia darasa kama ofisi na suala hilo kuwapa changamoto kubwa  

Mwarwa chacha Maligili ni diwani wa kata ya Binagi Wilayani Tarime Mkoani Mara amedhibitisha kutokaea kwa tukio hilo nakusema kuwa tukio hilo kutokea shuleni hapo  ni mara ya pili  huku akiomba serikali na wadau ambao wamesomea shule hiyo kuchangia kwa lengo la kujenga na kumalizia maboma yaliyopo ili kuwanusuru wanafunzi hao kwani mvua zilizoanza kunyesha hata majengo yaliyobaki siyo rafiki.

“Tukio hili la kuezuliwa kwa madarasa katika shule hii ya nyamwigula ambayo inasoma kwa hawamu na shule ya msingi Tumaini  yamekuwa yakitokea mvua kali zinaponyesha pale zinapoambatana na upepo na pia majengo haya yamejengwa kwa muda mrefu zile enzi za vijiji sasa waanchi wameanza kujitolea kujenga vyumba vinne na ofisi ya walimu kwa kuwaamasisha na kuwaomba wadau serikli ikatuunge mkono” alisema Diwani.

Diwani huyo aliongeza kuwa serikali pamoja na wadau wa maendeleo wajitokeze kwa wingi ili kusaidia shule hizo na majengo ya zamani yaweze kubomolewa ili kujenga ambayo ni bora kwa lengo la kuepusha hatari ambayo inaweza kutokea badae.

Paul Magele ni Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwigula na Mrimi Malisa Mwenyekiti wa kamati ya Maendeleo wakieleza  jitihada zilizopo kwa lengo la kutatua changamoto hiyo walidai kuwa kwa sasa jujkumu lililopo ni kuitisha mkutano wa wanachi ili kuzungumzia changamoto na ikiwezekana waanze kuchania kwa lengo la kujenga maboma ya madarasa.
DARASA LILILOBOMOLEWA
MOJA YA MADARASA AMBAYO YANATUMIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI NYAMWIGULA NA TUMAINI KATA YA BINAGI WILAYANI TARIME MKOANI MARA
MASHAMBA YALIVYOHARIBIWA NA UPEPO MKALI

Powered by Blogger.