MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSIANA NA WAUZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya
Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam
iliyofanyika jana.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akimkabidhi zawadi Mkaguzi wa Polisi, David Mabula.Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani
Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi
ya pikipiki kutokana na ufanyakazi bora.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau
kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kupambana wa waingizaji na
wauzaji wa dawa za kulevya nchini.
Mwigulu alitoa kauli hiyo wakati
akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa
Kinondoni jijini Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.
"Serikali imejipanga kupambana na
dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la kitaifa ambapo vijana wengi
wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.
Mwigulu alisema serikali ya awamu ya
tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye kwamisha jitihada za
kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga kuupunguza kwa asilimia 10
ifikapo mwaka 2019.
Aliongeza kuwa kanuni na sheria
zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani ya jeshi la polisi
zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi.
Akitolea mifano kadhaa alisema askari
polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi hilo anapaswa kupewa fedha
za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na suala hilo si la kumuonea
huruma askari husika bali ni haki yake.
Alisema kwa upande wa askari polisi
aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa mapambano dhidi yake na wahalifu
askari huyo anapaswa kulipa fidia yake kwa wakati badala ya kuunda tume
ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa katika mapambvano hayo.
"Mambo mengine hayahitaji mpaka uwe
na elimu kubwa askari amepambana na majambazi mbele ya watu lakini
majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake anashindwa kulipwa eti mpaka
iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji Mwigulu.
Alisema kwa muda mrefu askari
anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia kwa nauli na fedha za
kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila ya sababu za msingi.
Alisema hali hiyo kama askari husika
anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza katika tamaa na kutumia silaha
aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba wahusika kuliangalia jambo hilo
kwa karibu kwani mshahara na posho kwa askari hao ni haki yao.
Mwigulu alisema serikali kupitia Rais
Dk. John Magufuli imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa askari polisi
ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba na kuona namna ya kubadilisha sheria
ambazo zinaonekana hazina tija kwa wakati huu katika kuliongoza jeshi
hilo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)